GET /api/v0.1/hansard/entries/1071779/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1071779,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1071779/?format=api",
    "text_counter": 27,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Endebess, JP",
    "speaker_title": "Hon. (Dr.) Robert Pukose",
    "speaker": {
        "id": 1458,
        "legal_name": "Robert Pukose",
        "slug": "robert-pukose"
    },
    "content": " Asante Mheshimiwa Bwana Spika. Nataka kuunga mkono lile Ombi ambalo limetolewa na Mheshimiwa Mbalu kwa mambo ya wanyamapori. Kule Endebess tuko na Mbuga ya Mt. Elgon. Na katika hiyo mbuga unakuta kwamba wanyamapori wanakula mahindi na mimea mingine ya wakaazi wa kule. Unapata kwamba pia kuna ile inaitwa ngiri. Ngiri pia wanakula yale mahindi lakini kufidia inakuwa shida. Kwa hivyo, ningependa kamati inayohusika wanapopitisha bajeti ya Wizara ya Wanyamapori waangalie waone kwamba kuna mpango wa kuweza kufidia yale... Hii ni kwa sababu Bunge hili mwaka wa 2016 lilipitisha sheria. Katika sheria hiyo kuna fidia ya wewe ukiumia kwa mambo ya ndovu ama wanyamapori wakiharibu chakula cha wananchi. Kwa hivyo, ni vizuri waangalie katika hiyo bajeti kwamba wizara iko na pesa ambazo inaweza kufidia wakulima na wale wengine wanaoumia. Asante Bwana Spika."
}