GET /api/v0.1/hansard/entries/1072181/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072181,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072181/?format=api",
    "text_counter": 31,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kipipiri, JP",
    "speaker_title": "Hon. Amos Kimunya",
    "speaker": {
        "id": 174,
        "legal_name": "Amos Muhinga Kimunya",
        "slug": "amos-kimunya"
    },
    "content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda naomba kuwakilisha Hoja ifuatayo: KWAMBA, kwa mujibu wa Kanuni ya 25 (Mgeni Mashuhuri), Shukrani za Bunge la Taifa zinakiliwe kwa ajili ya Hotuba ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyotolewa katika Kikao cha Pamoja cha Bunge la Jamhuri ya Kenya mnamo Jumatano, tarehe 5, Mei, 2021. Mnamo Jumatano, tarehe 5 mwezi huu wa Mei mwaka huu wa 2021, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyekuwa katika ziara rasmi ya hapa Kenya kwa mwaliko wa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta alihutubia Bunge hili katika kikao cha pamoja tukiwa Bunge la Taifa na Bunge la Seneti. Kikao hiki kilifanyika kwa mujibu wa Kanuni zetu za Bunge ikiwa Kanuni 25 ya Bunge la Taifa na Kanuni 26 ya Bunge la Seneti. Mhe. Rais Suluhu Hassan alitoa Hotuba ya ufasaha, ya kueleweka na yenye ujumbe mzito kwetu sisi tukiwa Wabunge wanaowakilisha wananchi wa Kenya na haswa kwa sababu ya uhusiano wa mataifa yetu mawili. Alitoa mifano mingi na kuchora taswira iliyofanya ujumbe wake ueleweke kwa wepesi. Pia alitufunza mengi haswa katika lugha ya Kiswahili. Alitupatia misamiati ya kutosha, sasa tunajua “ushoroba wa pwani” unamaanisha “ coastal corridor” . Kabla ya siku hiyo, ni Mhe. Naomi Shaban aliyekuwa anaulewa msamiati wa ushoroba wa pwani. Pia majina kama “adhimu” na “rea” yalitumika. Heshima adhimu aliyopewa na Rais and rea ni respect . “Mikakati hasi” ina maana ya negative measures or strategies ambazo hazisaidii. Kuna mafundo ambayo sijui kama Kiongozi wa Chama cha Walio Wachache anaweza kutuelimisha kwa sababu kama unavyoona, ameingia mitini. Rais Suluhu pia alituonyesha vile amejitahidi kueneza na kutetea lugha ya Kiswahili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Hotuba ya Rais Hassan ilisheheni mambo mengi lakini kwa sababu ya uchache wa muda naomba nitaje maswala mawili. Swala la kwanza ni umoja wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}