GET /api/v0.1/hansard/entries/1072182/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072182,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072182/?format=api",
"text_counter": 32,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kipipiri, JP",
"speaker_title": "Hon. Amos Kimunya",
"speaker": {
"id": 174,
"legal_name": "Amos Muhinga Kimunya",
"slug": "amos-kimunya"
},
"content": "mataifa yetu mawili au utangamano tukielewa kwamba tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki tukiwa nchi sita; Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi, Rwanda na pia Sudan Kusini. Kuhusu Kenya na Tanzania Rais alisisitiza kuhusu umoja wetu, tumeshikana kidamu. Sisi ni ndugu wa damu, tumeshikana kupitia historia na jiografia yetu kwa sababu tuna mipaka ambayo huwezi ukaelewa kama uko kusini mwa Kenya ama Kaskazi mwa Tanzania. Ukiwa Arusha na usafiri hadi Taveta unaona hawa watu wote wanashirikiana vizuri. Wao ni jamii na wameshirikiana kwa damu. Hakuna haja ya sisi kutengana kisiasa. Alitushauri tudumishe huu undugu wetu na akasema, kwake yeye na katika awamu yake ya uongozi, atahakikisha kuwa Kenya inabaki kuwa ndugu, jirani na mshirika wa kimikakati na mbia."
}