GET /api/v0.1/hansard/entries/1072183/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072183,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072183/?format=api",
"text_counter": 33,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kipipiri, JP",
"speaker_title": "Hon. Amos Kimunya",
"speaker": {
"id": 174,
"legal_name": "Amos Muhinga Kimunya",
"slug": "amos-kimunya"
},
"content": "Suala la pili ni himizo lake Rais kwamba Bunge liwezeshe biashara kati ya nchi zetu mbili na kuendeleza ushirika kwa jumla tukikumbuka kwamba tuko katika soko huru ambalo ni la nchi hizi sita. Katika mkataba uliowekwa wa kuunganisha nchi hizi na kufungua soko huru, kuna uhuru wa watu kutembea na kufanya biashara. Unaweza kwenda Tanzania kuanzisha biashara na Mtanzania akatoka Tanzania akaja hapa Kenya akaanzisha biashara. Uganda vile vile. Unaweza kununua ardhi na kufanya kazi popote lakini kumekuwa na tatizo. Nilivyomusikia, alisema wakati umefika wa sisi kusema, \"Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyo sasa na yajayo\". Huu ni ukurasa mpya ambao tunaona unafunguka. Ni sura mpya inafunguka katika ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Kuhusu biashara kati ya nchi hizi zetu mbili, Rais Saluhu Samia Hassan alisema kwamba anaona wafanyabiashara wako mbele. Wametembea hatua kadha mbele ya sisi Wabunge na serikali. Wao wenyewe wametutangulia na ni lazima sisi tukiwa serikali au Wabunge, tuanze kuangalia ni vipi sera na sheria zetu zitawafikia. Hivyo, tutaweza kufanya biashara bila matatizo. Anatuhimiza sisi viongozi katika Bunge na mahakama kuwaonyesha wananchi wetu njia. Tusiwafungie njia za maendeleo na ustawi wao. Mhe. Naibu Spika wa Muda, mimi nafurahia kwamba kupitia uongozi wa Spika wa Bunge letu, Bunge la Taifa na lile la Seneti limepitisha sheria za biashara zinazojulikana kwa kimombo kama Business Laws (Amendment) Bills. Wazo la Mheshimiwa Rais wa taifa letu limekuwa kurekebisha sheria ambazo zinalemaza biashara. Tumewasilisha Mswada mmoja hapa leo wa kueleza vile wawekezaji wa kibinafsi wanaweza kuhusika kwenye miradi ya maendeleo ya umma. Hizo zote tunafanya ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya biashara zao katika hali na mazingira ambayo yatawastawisha bila wao kupata matatizo. Hivyo basi ni lazima tufuatilie suala la Mheshimiwa Rais ama kwa utunzi wa sheria au maswali kwa Serikali. Mimi ningependa kumshukuru Rais Suluhu Hassan kwa uamuzi wake. Inaonekana wazi amejitolea. Anataka kutatua yale matatizo ya watu kuchukiana hasa kati ya sisi Wakenya na Watanzania. Anataka kuondoa hiyo chuki. Ni njia moja ya kupalilia magugu ambayo yanakua na kuzuia mbegu ambayo ilipandwa ya uhusiano bora. Sharti tuweze kufanya biashara na kuketi kama ndugu. Haya magugu yaliingia na yakaanza kuharibu mahusiano baina yetu. Inaonekana yeye, akishirikiana na Rais wetu Mhe. Kenyatta, wataweza kupalilia hayo magugu ndio uhusiano wetu usiwe mashakani siku za usoni. Labda nitaje kwamba nilifurahia kumsikia Rais Suluhu akitupatia hongera kwa kutafsiri Kanuni zetu za Kudumu katika lugha ya Kiswahili. Juhudi hizi na nyinginezo za kuleta Kiswahili Bungeni zitakuwako. Zitakuza matumizi ya Kiswahili Bungeni. Leo nafurahia kuwaona Wajumbe wengi wakiwa hapa. Kuna wataalamu wa lugha na kuna wengine ni lugha yao ya kwanza. Kwa hivyo, sote kwa pamoja tunaweza kukitumia Kiswahili sio tu katika siasa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}