GET /api/v0.1/hansard/entries/1072184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072184,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072184/?format=api",
"text_counter": 34,
"type": "speech",
"speaker_name": "Kipipiri, JP",
"speaker_title": "Hon. Amos Kimunya",
"speaker": {
"id": 174,
"legal_name": "Amos Muhinga Kimunya",
"slug": "amos-kimunya"
},
"content": "huko mitaani bali pia katika utunzi wa sheria. Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Rais Suluhu kwa hotuba yake ya kipekee yenye wingi wa hoja na ujumbe wa aina yake. Naomba pia nitoe pongezi zangu kwa Rais wetu Uhuru Muigai Kenyatta, wewe Mhe. Spika, mwenzako Spika wa Seneti, Mhe. Kenneth Lusaka na Wabunge wa Bunge la Taifa na Wabunge wa Seneti kwa heshima waliomwonyesha Rais wa nchi jirani, Rais Suluhu Samia Hassan. Hilo lilifanya kikao hicho kikawa cha kihistoria. Ni kikao cha kupigiwa mfano kwa viongozi watakaokuja siku za usoni. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kuhitimisha kwa heshima, naomba kutoa Hoja na kumwalika Mhe. Naomi Shaban, akiwa mtaalamu wa lugha hii, aweze kuafiki Hoja hii."
}