GET /api/v0.1/hansard/entries/1072188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072188,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072188/?format=api",
    "text_counter": 38,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Taveta CWR, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Dkt) Naomi Shaban",
    "speaker": null,
    "content": " Ndio naendelea. Nitaeleza. Katika hali yangu ya kuafiki, natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kumwalika Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ambaye ndiye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Namshukuru haswa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutembele Bunge letu la Kenya. Ningependa kusema kuwa ndugu si kufanana tu bali ni kufaana. Ndugu wa Kenya na Tanzania ni ndugu ambao wamezaliwa... Kama vile Mheshiwa Rais Suluhu Hassan mwenyewe alivyosema, kutengana kwetu hakuwezekani kwa sababu sisi ni ndugu wamoja. Mimi natoka maeneo ya mpakani. Haswa tunapakana pale Taveta na Holili upande wa Tanzania. Sisi ni ndugu kwa sababu ndugu zetu wengine wamevuka mpaka wako upande ule mwengine. Wengine kutoka Tanzania wako upande wetu. Vile vile ndugu wa Kenya wameolewa na wameoa... Vile vile, ndugu wa Kenya wameolewa na wameoa Tanzania. Hivyo basi, kama vile Mhe. Raisi Samia Suluhu alivyosema, mimba yaweza tungiwa Kenya ikazaliwa Tanzania. Ukweli wa mambo ni kuwa, hospitali ya karibu pahali ambapo huwa tunatuma wagonjwa kukiwa kunahitajika matibabu zaidi ni upande wa Tanzania, Kilimanjaro Christian Medical Center ambayo iko upande ule, kwa sababu ndiyo iko karibu kushinda kuenda Voi ambako hutuchukua safari ndefu. Katika hali ya kukaa pale mipakani, hatuwezi kugawa hali ya uchumi wetu kwa sababu hakuna uchumi wa mpaka huu ama mpaka ule. Wakulima wetu wanauza bidhaa zao, haswa vyakula wanavyovuna mashambani, upande ule mwingine na wale pia wanauza bidhaa zao upande huu. Hivyo basi, Mhe. Rais katika hotuba yake akitaja mpaka wa Taveta na Holili ambako kuna ile inatwa kwa Kingereza one-stop-boarder, pahali pamoja pakufanyia shughuli za mipakani, kazi zinazoendelea pale zinaleta faida kwa watu wetu kutoka pande zote mbili. Ningependa kutaja kuwa, sisi tunaotoka mpakani kama Taveta, Mwaka wa 2015 nataka kuwakumbusha kuwa Mhe. Raisi Uhuru Kenyatta alimualika Mhe. Rais Jakaya Kikwete kule Taveta kabla hajamaliza awamu yake. Wakati huo, wakaanzisha ile barabara inayoelekea upande wa Voi. Haya yote yalitendeka kwa sababu ya uhusiano mzuri ulioyoko kati ya Kenya na Tanzania. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}