GET /api/v0.1/hansard/entries/1072189/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072189,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072189/?format=api",
"text_counter": 39,
"type": "speech",
"speaker_name": "Taveta CWR, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Dkt) Naomi Shaban",
"speaker": null,
"content": "Vile vile, namshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa sababu mwanzo wa ziara zake, ameona kuwa aweke Kenya mbele aipatie nafasi ya awali ili aweze kututembelea. Haya yote hayangewezekana kama siyo uhusiano wetu mzuri ambao una mizizi mirefu sana. Hata Kanuni za Kudumu za hapa Bungeni zilizinduliwa na Bunge la Muungano wa Tanzania. Hatuyachukulii maswala haya kama mchezo. Haya ni maswala ya undugu ambayo tutazidi kudumisha. Ningependa vile vile, kushukuru kuwa Mhe. Rais Mwendazake, John Pombe Magufuli aliamua kumpatia nafasi mama Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa naibu wake. Sasa hivi ndio amepata nafasi hiyo ya kuwa Rais. Alionyesha heshima kubwa kwa akina mama. Vile vile, ningependa kuwashukuru Watanzania kwa hali ya utulivu waliyokuwa nayo kumpokea Rais Suluhu Hassan. Heko kwao. Ningependa kuchukua nafasi hii kama Mbunge wa Taveta kutoa pole kwa kumpoteza Rais jirani wetu, lakini vile vile, kwa sababu nilikua Waziri aliyehusika na mambo ya jinsia, kufurahia kuwa Mama Suluhu amepata nafasi hiyo."
}