GET /api/v0.1/hansard/entries/1072197/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072197,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072197/?format=api",
    "text_counter": 47,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Nominated, JP",
    "speaker_title": "Mhe. David ole Sankok",
    "speaker": {
        "id": 13166,
        "legal_name": "David Ole Sankok",
        "slug": "david-ole-sankok"
    },
    "content": " Naomba uniongezee dakika zangu. Ningependa kumshukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kutuletea Suluhu hapa nchini Kenya. Tulipata suluhu ya ng’ombe zetu kutopigwa mnada hata kama zitavuka mpaka bila pasipoti. Tulipata suluhu za vifaranga kutoteketezwa hata kama watapatikana nchini Tanzania bila pasipoti. Tulipata suluhu ya miundo mbinu za kidiplomasia, ushirikiano, maendeleo na amani. Mhe. Suluhu karibu tena nchini kwa sababu nchi hii ina uhuru; uhuru wa kujieleza, wa kuabudu, kutembea, kuishi na kufanya biashara popote nchini na uwezekano wa vipaji. Mhe. Suhulu, vile nyumbu wa Serengeti wanavyovuka mipaka kutungwa mimba Maasai Mara, ndivyo Wakenya na Watanzania watavuka mipaka kuekeza na kufanya biashara katika nchi zote mbili. Vile nyumbu wa Tanganyika wanavuka mipaka kutafuta mapenzi Maasai Mara bila pasipoti ndivyo Wamaasai wa Kenya watavuka mipaka kutavuta wamaasai wenzao Tanzania bila masharti. Vile wanyama wa Serengeti wanatembeleana na wenzao wa Mara bila pasipoti, ndivyo waendeshaji wa utalii watatembea kuenda Tanzania bila vikwazo vyovyote ili The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}