GET /api/v0.1/hansard/entries/1072198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072198,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072198/?format=api",
"text_counter": 48,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nominated, JP",
"speaker_title": "Mhe. David ole Sankok",
"speaker": {
"id": 13166,
"legal_name": "David Ole Sankok",
"slug": "david-ole-sankok"
},
"content": "tuimarishe biashara ya utalii. Vile Nyumbu wa Serengeti wanatungwa mimba Maasai Mara na kuzalia Tanzania, ndivyo ng'ombe wa wamaasai watatungwa mimba huku Kenya na kuzalia Tanzania bila masharti yoyote. Mtukufu Rais Suluhu Hassan, ni heshima kubwa sana nikiwa mwakilishi wa wakenya walemavu kuwa mmoja wa Wabunge ambao walisikiza hotuba yako kwa vikao vya pamoja vya Bunge la Seneti na Bunge la Taifa. Ilikuwa heshima kubwa sana na nashukuru sana. Kuwa mama wa kwanza kuwa Rais Afrika Mashariki ni ishara tosha kuwa watu wetu wanadhamini vikundi maalum vya riba, special interest groups kwa kimombo. Kwa mapenzi ya Maulana, mkenya mlemavu atakuwa rais hivi karibuni. Rais Suluhu Hassan, nakubaliana nawe kwamba Kiswahili chetu sio murua kama chenu. Kiswahili chetu kina vioja na vitimbi. Tulipoanzisha rasmi Kiswahili Bungeni, mimi, Mhe. David ole Sankok, nilifikiri Standing Orders zinatafsiriwa kama “Amri ya Kusimama”. Naomba msamaha. Nimejikakamua tangu tuanzishe Kiswahili Bungeni mpaka sasa at least, nimeweza kuongea Kiswahili na nafikiri nitapata alama ya “A”. Asante, naunga mkono."
}