GET /api/v0.1/hansard/entries/1072202/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072202,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072202/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Suba North, ODM",
    "speaker_title": "Mhe. (Ms.) Odhiambo-Mabona",
    "speaker": {
        "id": 376,
        "legal_name": "Millie Grace Akoth Odhiambo Mabona",
        "slug": "millie-odhiambo-mabona"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kiswahili sio mdomo wangu lakini nitaongea leo ili nipongeze mama mwenzangu. Ninajiona mwenye bahati kubwa kupewa nafasi hii adimu na ya kipekee kuongea kuhusu hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan. Hapo nimeongea sawa au sio? Inanikumbusha wakati nilikuwa shule ya msingi ya Homa Bay ambapo Jumatano ilikuwa siku ya kuongea kwa Kiswahili. Watu wengi walikuwa wananyamaza. Wale waliopenda kuongea sana kama mimi walikuwa wananyamaza na kwa wale waliokuwa wanapenda kunyamaza, walikuwa wanaongea. Kwa hivyo, leo tutaona ni akina nani huwa wananyamaza. Leo watajiinua kwa sababu wanajua hatujui Kiswahili, sasa watataka kutushtua. Hio ni sawa au sio sawa? Mhe. Naibu Spika wa Muda, nataka kukubaliana na Rais Suluhu Hassan aliposema kuwa sio kila rais anayefanya ziara rasmi hupewa heshima ya kuhutubia Bunge, tena kikao cha pamoja cha Bunge zote mbili. Tumefurahi, sana sana mimi kama mama Mbunge. Ninamrudishia shukrani kwa kututembelea na namrudishia shukrani Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kumwalika kuja Kenya. Kama mama kiongozi, nilifurahi zaidi kwa sababu yeye ndiye mama wa kwanza Afrika Mashariki kuwa rais. Watu wa Suba North na Tanzania wanashirikiana mpakani mwa Ziwa Victoria. Mara nyingi wavuvi wetu wanashikwa Tanzania. Naomba Rais wetu Mhe. Uhuru Kenyatta aendelee kujadiliana na Rais wa Tanzania ili tusiwe na shida tukifanya uvuvi. Mimi kama mama kiongozi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}