GET /api/v0.1/hansard/entries/1072205/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072205,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072205/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Isiolo CWR, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Ms.) Rehema Jaldesa",
    "speaker": {
        "id": 601,
        "legal_name": "Rehema Dida Jaldesa",
        "slug": "rehema-dida-jaldesa"
    },
    "content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii kuchangia mjadala ambao ni muhimu sana, hasa kwa mtu kama mimi ambaye nimetoka kwa jamii ndogo. Nimeweza kupata nafasi ya kuona dada yangu ambaye ni Rais wa pekee katika jumuiya ya Afrika. Hiyo imenifurahisha sana. Nataka nichukue nafasi hii kumshukuru Rais wetu Mhe. Uhuru Kenyatta kwa kumualika Rais Samia Suluhu Hassan. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Rais Suluhu Hassan aliongea mengi ambayo ni muhimu kwa sisi Kenya na pia nchi ya Tanzania. Kwanza, aliongea kwa ukarimu sana na utulivu pia. Aliweza kuonyesha ujuzi mwingi kwa yale mambo alikuwa anayasema. Aliongea mengi kuhusu nchi zetu mbili. Kwanza, aliweza kuongea mambo ya uboreshaji wa biashara kati ya nchi zetu mbili. Pili, Rais aliweza kuleta uhusiano bora katika Kenya na Tanzania. Alisisitiza kuwa sisi tumehusiana kwa damu na kijirani pia. Hayo ni mambo ambayo ni muhimu. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kuna wale ambao wametoka kwa jamii ndogo. Mimi ni kiongozi wa Kiislamu ambayo ni jamii haijawahi kukubali uongozi wa akina mama. Rais Suluhu Hassan alikuja Kenya na kuhutubia Bunge letu. Hii ilipeleka graph yetu juu kama viongozi akina mama. Hilo ni jambo siwezi kuchukua rahisi. Imeonyesha ya kwamba sisi, wamama, tunaweza. Aliongea na ujuzi mwingi. Lakini, hapo alikuwa pia anawaonyesha upole. Kwa hivyo, ni jambo ambalo limefurahisha Kenya na dunia nzima. Kama kiongozi mama, nimefurahi sana. Namuombea Mwenyezi Mungu aendelee kuwasha nyota yake."
}