GET /api/v0.1/hansard/entries/1072223/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072223,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072223/?format=api",
"text_counter": 73,
"type": "speech",
"speaker_name": "Igembe North, JP",
"speaker_title": "Mhe. Maoka Maore",
"speaker": {
"id": 13344,
"legal_name": "Richard Maore Maoka",
"slug": "richard-maore-maoka"
},
"content": " Namshukuru Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mhe. Suluhu Hassan. Ni baraka kutoka kwa Mungu kuwa na jirani ambaye mnaheshimiana. Ni baraka kutoka kwa mungu kuwa na jirani mwema ambaye ako na manufaa mengi sana. Jirani mwema akiona unanawiri, anafurahia. Tulipokuwa shuleni, tulikuwa na watu kutoka Tanzania ambao walikuwa mashuhuri. Walikuwa wameandika vitabu ambavyo tulikuwa tunavisoma shuleni kama vile Shaaban Robert. Kuna wale wanajua kutunga mashairi kwa mfano, “Titi la Mama Litamu hata Likiwa la Mbwa’’ . Pia, kuna mwingine mashuhuri anaitwa Ibrahim Hussein ambaye ameandika mchezo wa kuigiza ambao unaitwa Mashetani . Kuna msemo ambao naupenda sana na ningependa kuutumia leo: “Mpanda ngazi na mshuka ngazi hawawezi kushikana mikono.” Kwa sababu hiyo, Rais Suluhu Hassan alipowasili hapa, alikuja ili tushikane mikono ndio tuweze kusonga mbele pamoja kiuchumi, kimaendeleo na kidiplomasia. Vile vile, alipotutembelea hapa katika ziara yake, nilipata simu nyingi nikiambiwa kwamba Tanzania haina sheria ambazo zinaweza kuharibu biashara nyingi. Kuna mumea The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}