GET /api/v0.1/hansard/entries/1072224/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072224,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072224/?format=api",
    "text_counter": 74,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Igembe North, JP",
    "speaker_title": "Mhe. Maoka Maore",
    "speaker": {
        "id": 13344,
        "legal_name": "Richard Maore Maoka",
        "slug": "richard-maore-maoka"
    },
    "content": "tunaopanda kule kwetu unaoitwa ‘ miraa ’ ama ‘ maurungi ’ kama unavyojulikana huko. Ni vizuri kusema kuwa hapa Kenya, mumea huu ni biashara halali. Lakini ukivuka mpaka upande wa Tanzania, biashara ya miraa ni haramu. Mara nyingi nimejaribu kuwatoa vijana jela kule wakiwa wamefungwa maisha kwa sababu ya kujihusisha na biashara ya miraa . Tunasema kuwa huu ndio wakati wa kupeleka ujumbe kule pole pole ili tujitetee kidogo tusiwe tunaumia. Bi. Naibu Spika wa Muda, kabla ya kuaga dunia kwa Hayati Rais John Pombe Magufuli, hatukuwa tunamfahamu Makamu wa Rais wa Tanzania. Alivyochipuka na kuchukua usukani, wengi walipomskia, waliona ni kiongozi ambaye amejaa taadhima, hekima na ni mwerevu wa akili kuliko viongozi wengi tuliowahi kuwasikia. Rais Suluhu aliweza kuwasisimua Wakenya kwa njia nyingi. Afrika Masharika imepunga hewa tofauti na tunamsifu Mungu kwa kutuletea kiongozi kama huyu kututembelea hapa nchini Kenya. Ahsante, Bi. Naibu Spika wa Muda."
}