GET /api/v0.1/hansard/entries/1072231/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072231,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072231/?format=api",
    "text_counter": 81,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Narok CWR, JP",
    "speaker_title": "Mhe. (Ms.) Soipan Tuya",
    "speaker": {
        "id": 926,
        "legal_name": "Roselinda Soipan Tuya",
        "slug": "roselinda-soipan-tuya"
    },
    "content": " Mhe. Bi. Naibu Spika wa Muda, utaniongezea muda wangu kwa sababu amenikatiza kwa njia isiyo halali. Tunahitaji kuthibitisha kama kweli ni maji ama ni kitu kingine. Nilikuwa nasema kwamba niko na furaha sana kama mama kiongozi; mama ambaye ako na watoto wa kike, ambao ndio viongozi wa kesho. Hatua ambayo wamechukua Watanzania, ingawaje uongozi wa Rais Suluhu ulikuja kwa njia ya kipekee ambayo ni ya kusikitisha, akiwa mama kiongozi ambaye anaona mwanga mpya ambao unaangazia uongozi wa kina mama, nina furaha sana. Unaposoma vichwa vya habari kuhusu uhusiano mwema Afrika Mashariki kwenye mambo ya uwekezaji, maendeleo na biashara, tangu Rais Suluhu kushika usukani, umekuwa ni muda mfupi sana lakini tayari tumeshaanza kuona anga mpya na mwamko mpya katika uhusiano mwema kati ya Kenya na Tanzania. Uhusiano huu pengine utafungua nafasi nyingi za kuweza kuendeleza uwekezaji na ujirani mwema. Haya ni maneno ambayo yataleta mambo mazuri na yanapitia katika uongozi wa mama. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}