GET /api/v0.1/hansard/entries/1072232/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072232,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072232/?format=api",
"text_counter": 82,
"type": "speech",
"speaker_name": "Narok CWR, JP",
"speaker_title": "Mhe. (Ms.) Soipan Tuya",
"speaker": {
"id": 926,
"legal_name": "Roselinda Soipan Tuya",
"slug": "roselinda-soipan-tuya"
},
"content": "Uongozi wa Rais Suluhu Hassan unatuonyesha kwamba wakati wa akina mama umefika. Kwa lugha ya Kimombo, tunasema “ We should rise to the occasion. We should wake up andsmell the coffee ” kwa sababu wakati wa kina mama umefika. Nikiangazia nyanja mbali mbali, leo asubuhi tuliweza kumkagua aliyeteuliwa kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu wa Mahakama ya Kenya. Hili ni jambo ambalo halijasikika kihistoria katika nchi hii yetu. Hata katika nyadhifa nyingine nyingi, tunaona nafasi ya kina mama inazidi kupanuka na kuongezeka. Rais Suluhu alizuru nchini Kenya ikiwa ziara yake rasmi ya kwanza tangu achukue hatamu za uongozi nchini Tanzania. Hiyo ni heshima kubwa sana kwa Kenya, na shukrani kwa Mhe. Rais Uhuru Kenyatta kwa kumpa fursa hiyo. Hii ni njia moja ya kuonyesha kwamba Kenya tunatambua uongozi wa kina mama na tunajua wanaweza. Na wale ambao wanaendeleza mijadala na fikira za kusema kwamba kina mama hawawezi, nafikiri wanaendelea kuota ndoto ya mchana. Nawasihi Wakenya wote, Wanaafrika Mashariki, Wanaafrika na dunia nzima; tuwape kina mama uhuru wa kuweza kuingia katika nyanja zote za uongozi kwa sababu wanaweza, na tutakuwa na matumaini. Hata watoto tunaolea watajua kwamba ndoto zao ni halali bila kujali kama yeye ni msichana au mvulana. Asante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda."
}