GET /api/v0.1/hansard/entries/1072235/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072235,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072235/?format=api",
"text_counter": 85,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyando, ODM",
"speaker_title": "Hon. Jared Okelo",
"speaker": {
"id": 13457,
"legal_name": "Jared Odoyo Okelo",
"slug": "jared-odoyo-okelo-2"
},
"content": " Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwanza kabisa, wacha nikushukuru kwa kunipa nafasi hii niweze kuongeza sauti yangu katika Hoja hii ya mjadala huhusu hotuba ya Mhe. Suluhu ambaye ni Rais wa Tanzania aliyoitoa hapa Bungeni kwetu. Kuja kwa Mhe. Suluhu katika Jengo hili, ni kuonyesha heshima kubwa sana kwa Wabunge wa Taifa la Kenya. Tunamshukuru kwa kupata nafasi ya kuja kwetu kututembelea na kuzungumza maneno ambayo yana uzito katika uboreshaji wa maswala ya uchumi, elimu, mambo ya barabara na mengineyo. Sisi kama Wakenya ambao Mwenyezi Mungu ametupa nafasi kuwa hapa Bungeni, tunasema asante sana. Tuligundua kwamba Mhe. Suluhu ndiye Rais wa pili kuzungumza katika Jengo hili baada ya Rais wao wa awali, Mhe. Jakaya Kikwete, pia kupata nafasi mwafaka kama hiyo na kuzungumza nasi hapa nchini Kenya. Nchi zetu zimepakana na ni dhihirisho ya kufanana kwa utamaduni wetu kama ndugu na dada. Alizungumza maneno mengi sana juu ya undugu wetu. Tusionyeshe undugu huo tu kwa mambo ya Kenya na Tanzania lakini kwa bara la Afrika nzima na hata ikiwezekana, tuionyeshe katika dunia nzima. Akina mama wamekuwa na vita vikali sana dhidi ya kutopanda ngazi. Katika Karne hii ya 21, bado tunatatizwa na akina mama kutopanda nyadhifa za uongozi. Sasa tunasema kwamba Mhe. Suluhu kule Tanzania ametuonyesha kwamba akina mama wanaweza na kama Mungu atatujalia kwa huu wakati bado tunapumua hapa duniani, hata Kenya wakati fulani tupate mama atuongoze huku. Hii ni kwa sababu wameonyesha kwamba wanawake wanaweza. Juzi kule Ujerumani, tuliona wakati aliyekuwa Chancellor wao, Angela Merkel, alipomaliza kutoa hotuba yake ya kustaafu, kila mmoja alisimama na kumpigia makofi kwa dakika sita kwa kazi nzuri ambayo aliwafanyia. Hapa Kenya pia tuwape wanawake nafasi kutuongoza na tuwapigie makofi vile tuliona kule Ujerumani. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}