GET /api/v0.1/hansard/entries/1072236/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072236,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072236/?format=api",
"text_counter": 86,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nyando, ODM",
"speaker_title": "Hon. Jared Okelo",
"speaker": {
"id": 13457,
"legal_name": "Jared Odoyo Okelo",
"slug": "jared-odoyo-okelo-2"
},
"content": "Tukiwa hapa Bungeni na Mhe. Suluhu, tulichekeshwa. Kulikuwa na mbwembwe na nderemo alipotaja kwamba wanyama wa pori kule Tanzania huwa wanakuja Kenya kutiwa mimba na kurudi kule Tanzania kuzaa. Sasa kazi ya wanyama wetu hapa nyumbani ni rahisi aje? Kazi yao ni kutia tu mimba wanyama wa kike kutoka kule Tanzania na kurudi kuzaa. Sasa hiyo mzigo tunapeleka Tanzania. Tulikuwa na vichekesho sana hapa wakati Mhe. Suluhu alitutembelea. Tumekuwa na changamoto kadhaa katika uwekezaji wa mali na jinsi ya kufanya biashara hapa na kule Tanzania. Kila mtu anatambua kuwa cheti au kibali cha kufanya kazi kule Tanzania kimekuwa kizungumkuti na alisema kwamba atafanya chochote anachoweza kuondoa kizingiti chochote ili tukae kama ndugu. Pia kama kibali kinatakikana na Mkenya kufanya kazi Tanzania, anafaa kupewa na vilevile Watanzania pia wakitaka kibali kufanya kazi Kenya, wapewe kwa sababu sisi ni majirani, ndugu na jamii moja. Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi. Naona light yangu is"
}