GET /api/v0.1/hansard/entries/1072246/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072246,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072246/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
"speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
"speaker": {
"id": 13231,
"legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
"slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
},
"content": " Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nichangie Hoja hii ambayo imefana sana. Ninaanza kwa kumpa pongezi zangu mimi binafsi na ya akina mama wa Kenya kwa Mama Suluhu Samia kwa kupata nafasi ya kuongoza kama Rais wa kwanza mwanamke katika Afrika Mashariki na pia kuwakumbuka wahusika ambao walikubali kumpa nafasi ili kuwaongoza na kumwamini. Si rahisi kwamba Mhe. Suluhu angepewa nafasi na ninashuku kwamba wale wote waliohusika walikuwa wanaume. Kwa hivyo, hongera sana kwa Serikali ya Tanzania kwa kukubali Mhe. Suluhu awaongoze. Pia tunapongeza Serikali yetu ya Kenya kwa kukubali kumkaribisha Mhe. Suluhu hapa nchini alipozuru. Alipewa heshima na nafasi ya kutosha ndiposa akaja hapa Bungeni kuhutubia Bunge zote mbili na tukamsikiliza kwa hekima aliyonayo, umri ambao anao na kwa kazi ambazo amefanya. Siku nyingi anaonekana kwamba anaweza na anaelewa kazi yake. Mimi binafsi, nilimwona yule Rais kama mama ambaye anataka kuleta uhusiano ulio bora kati ya nchi hizi mbili na hata Afrika Mashariki kwa jumla. Najua kwamba imekuwa si rahisi sisi kama Afrika Mashariki kuongea pamoja na kufanya biashara pamoja. Mara nyingi nimesikia wafanyabiashara humu nchini wakilalamika kwamba wakifanya biashara humo Tanzania, wale wanafaidika kuliko sisi Wakenya. Sasa natumai kwamba wakati huu wa Mhe. Suluhu ambaye ataleta suluhu, ataweza kufanya Wakenya kufurahia biashara humo nchini Tanzania. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}