GET /api/v0.1/hansard/entries/1072247/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072247,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072247/?format=api",
    "text_counter": 97,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Baringo CWR, KANU",
    "speaker_title": "Hon. (Ms.) Gladwell Cheruiyot",
    "speaker": {
        "id": 13231,
        "legal_name": "Gladwell Jesire Cheruiyot",
        "slug": "gladwell-jesire-cheruiyot"
    },
    "content": "Kuna mambo mengi ambayo tumeona Mhe. Suluhu akiyafikiria, akiyapanga na tunaona kwamba tukimshika mkono, kuna mabadiliko yataonekana. Tunajua kwamba mimea ambayo inapandwa hapa nchini mara nyingi tunabadilishana katika biashara ya Kenya na Tanzania. Hata hivyo, wafanyabiashara wetu huwa wanalalamika kidogo kwa sababu wakati wanapanda mimea yao, wataona wale wameleta nyingi lakini wao hawawezi kupeleka yao kule. Hii inaleta kukosana kidogo. Lakini naona Mhe. Suluhu anafanya bidii na tunashukuru sana. Tunaomba pia katika hiyo hali, sisi akina mama kwa sababu tumepata bahati kupata Rais mwanamke kwa Afrika Mashariki, tusitumie hiyo nafasi vibaya, kujigamba wala kuonyesha dharau lakini tunapaswa kupeana heshima na kushika mkono Mhe. Suluhu atekeleze kazi yake ili kuonyesha kwamba akina mama pia wanaweza. Tunamwambia kwamba anapokaa pale, anawakilisha akina mama wengi sana hapa Afrika Mashariki na hata dunia nzima. Kwa hivyo, anapofanya kazi yake, anapaswa kujua kwamba sisi sote na dunia nzima tunamtazama ili tuweze kukubali uongozi wa akina mama. Katika ile hali, hata hapa Kenya Rais wetu ameona ni vyema kumpa nafasi mama mmoja kuwa Jaji Mkuu humu nchini. Ninaona amezungumuziwa na ni kana kwamba amekubalika. Naomba tu uapishaji wake ufanywe kwa upesi kidogo ili katika ule moyo wa kupata akina mama uongozini, pia tupate Jaji Mkuu hapa nchini ili pia yeye aweze kuwakilisha akina mama katika mahakama zetu kama vile Mama Suluhu anafanya kule Tanzania. Mhe. Suluhu alipoongea kuna msemo ambao alisema, sijui kama sisi sote tulisikiliza. Alisema kuwa deni ya wema ni wema. Kwa hivyo, wakitutenda mema sisi pia tutende mema kwao. Kwa hivyo, ninaunga mkono Hoja hii. Bi. Suluhu, Mungu akusaidie uweze kutekeleza kazi na kuonesha kuwa akina mama wanaweza. Asante sana Bi. Spika."
}