GET /api/v0.1/hansard/entries/1072249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072249,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072249/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Fafi, KANU",
"speaker_title": "Hon. Mohamed Abdikhaim",
"speaker": {
"id": 13329,
"legal_name": "Abdikhaim Osman Mohamed",
"slug": "abdikhaim-osman-mohamed"
},
"content": " Asante Naibu Spika wa Muda. Nimefurahi umenipa hii nafasi nichangie mjadala huu kuhusu hotuba ya Rais jirani, Suluhu, alipofanya ziara yake ya kwanza hapa Kenya. Katika dini yetu ya Kiislamu, Mtume, ṣallā -llāhu ʿalayhī wa-sallam, ametuambia kitambo sana kuwa mtu akitaka kwenda peponi, basi iko katikati ya miguu ya mama. Alisema hilo mara tatu. Kwa hivyo, sisi kama Waislamu tumekubali akina mama kuwa viongozi kama alivyo Mama Suluhu. Pia kuna suala la jinsia. Sisi Wabunge wa Taifa la Kenya, hayo masuala ya jinsia yalipofika humu Bungeni hatukufanikiwa kuyapitisha. Ningeomba akina mama wakubali kujipigia kura. Vile najua, tuko na akina mama shujaa kama vile Martha Karua ambaye alikuwa katika hili Bunge kwa muda wa miaka ishirini. Alijaribu kugombea kiti cha urais wa hii nchi. Tulikuwa na mama mwingine kutoka Kitui, anaitwa Ngilu. Alikuwa waziri. Kwa hivyo, kama Wakenya tunataka kukubali akina mama kuongoza, lazima tupate huo uongozi kutoka kwa akina mama wenyewe—wakubali kupigia wenzao kura. Kwa nini nimesema hivi? Sitini kwa mia ya wapigajikura hapa Kenya ni akina mama. Kama akina mama watakubali kupigia mama mwenzao kura tutapata Rais wa kike humu nchini. Suala la pili ningependa kuchangia ni kuhusu ufisadi. Mimi nimefanikiwa na Mungu kuwa na wasichana wanne. Niko na watoto saba. Nasema alhamdulillah . Wanne ni wasichana. Bado ninatafuta mke wa pili, wa tatu na wa nne. Dini yangu inakubali hilo. Kuhusu mambo ya ufisadi niliyotaka kuchangia, kama tunataka kupigana na ufisadi hapa Kenya ama tunataka The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}