GET /api/v0.1/hansard/entries/1072256/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072256,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072256/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Shinyalu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
    "speaker": {
        "id": 71,
        "legal_name": "Justus Kizito Mugali",
        "slug": "justus-kizito"
    },
    "content": " Niko mbali, halafu nabanwa. Nashukuru Bi. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ili niseme machache tu kuhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Serikali hiyo, Bi. Suluhu Hassan. Kwanza kabisa ningependa kumshukuru Rais wetu wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa sababu ilitokana na ule uhusiano wake mzuri na watu wa Jumuiya hii. Nafikiri ndilo lilimfanya Bi. Suluhu kuona kwamba ni muhimu aje hapa ili atengeneze uhusiano. Kwa hilo ningependa kusema shukrani. Kwanza kabisa ningependa kumshukuru huyo Mhe. Rais wa Tanzania kwa kubadilisha mwenendo. Kama mnavyojua, mahusiano kati ya Kenya na Tanzania kutoka mwanzo yalikuwa na mporomoko na mushkili—mipaparuzano, mikinzano mingi, ikitokana na mambo ya kutoelewana, taharuki, kuogopana namna hiyo na kusema kwamba Wakenya ndio wajuaji. Kwa hiyo ilikuwa ni mambo ambayo hayana msingi. Lakini Dkt. Bi. Suluhu ambaye ndiye Rais wa nchi hiyo amebadilisha na kuleta mwenendo ambao sasa ni sawa kuleta ukuruba, kuleta mahusiano mazuri kati yetu na wao ili tuweze kuweka msingi wa undugu ambao utatufaa zaidi katika siku nenda siku rudi, daima dawamu. Utadumu milele ili kusaidia watu wetu wafanye kazi pamoja kwa sababu ya soko kuu. Wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na Kati wakifanya biashara pamoja, tutakuwa na soko kubwa la kazi, kuuza mazao yetu na kufanya mambo yetu mengi ambayo yatakuwa yanatufaa sisi haswa katika kuleta vitega- uchumi vitakavyofaa kwa watu wetu. Muhimu ni kwamba, ulipomuona Mama Suluhu akizungumza hapa, alizungumza Kiswahili kizuri sana. Kiswahili chenye uletelezi, sahili, burudani nyingi, bashasha, vijembe vimejaa mumo kwa ndani. Tuliona kwamba Kiswahili hicho kilikuwa kizuri sana kikatuchangamsha. Nimeona Kiswahili kimewatia Wabunge wa hapa motisha. Naona Wabunge wanazungumza Kiswahili kizuri. Nimemuona yule anayetoka kule Nyanza, nimemuona dada hapa wa kutoka kule akisema Kiswahili kizuri sana. Nawaambia kwamba lugha ya Kiswahili ni nzuri na itatufanya tuwe na mahusiano mazuri sana Tanzania. Ningependa, kwa vile mama yule The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}