GET /api/v0.1/hansard/entries/1072257/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072257,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072257/?format=api",
    "text_counter": 107,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Shinyalu, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Justus Kizito",
    "speaker": {
        "id": 71,
        "legal_name": "Justus Kizito Mugali",
        "slug": "justus-kizito"
    },
    "content": "ametutia motisha na mshawasha wa kuwa na uchu na tamaa ya kuendeleza lugha hii katika Bunge hili, itatufaa sisi pia tupate siku moja au mbili katika zile kaida ama Kanuni zetu ili tuweze kuzungumza Kiswahili kwa lazima. Tunapofanya mazoezi pale-hapa, tutakuwa tunazungumza sawasawa. Nilipomuona Mama Mhe. Rais akisema kwamba Kiswahili chetu kinakuwa na vituko na vijembe vinavyowafanya wacheke na kufurahia kinapozunguzwa, nafikiri ni sawa. Nataka niwaambie Wakenya wajue kwamba taifa letu la Kenya, katika ustandadi wa Kiswahili, tunaposema waandishi ambao wamekomaa, wale gwiji wanaojua lugha ya Kiswahili undani, wale wakiritimba, ni walewale wanaotoka hapa. Ningependa kuwashangaza kuwa yule anayezungumza Kiswahili kizuri zaidi, yule gwiji au bingwa mkubwa anatoka Nyanza. Anaitwa James Ndeda, ama muite Wallah bin Wallah. Ndiye muandishi wa mno katika lugha ya Kiswahili. Namshukuru Bibiye Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano, na Rais wa Kenya. Nasema asante, shukrani, naunga mjadala huu mkono wa dhati. Asante."
}