GET /api/v0.1/hansard/entries/1072274/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072274,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072274/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Gatanga, JP",
"speaker_title": "Hon. Joseph Nduati",
"speaker": {
"id": 13338,
"legal_name": "Joseph Nduati Ngugi",
"slug": "joseph-nduati-ngugi-2"
},
"content": " Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi niseme machache. Mimi naona unafanana na Rais wa Tanzania aliyetutembelea hivi majuzi. Nakuombea mazuri hata wewe ukuwe Rais wa Kenya siku moja. Lingine ni kushukuru sana Rais wa Tanzania kwa kututembelea na kusema yale aliyosema katika Bunge letu. Kutembea kwake hapa Kenya kutawezesha kuimarisha biashara kati ya watu wa Kenya na watu wa Tanzania. Tunawajua Watanzania kama wafanyabiashara kama Wakenya wenzetu. Na wanajulikana sana. Vyakula vingi hapa Nairobi hutoka pale Tanzania, kama mahindi na kitungu. Kwa hivyo, hiyo italeta bei ya chakula chini. Nawaambia wakulima wetu wafanye bidii pia waweze kuuza vitu vingine pale Tanzania. Lingine, ningependa kushukuru Rais kwa sababu ameuimarisha uhusiano wetu. Hapo mbeleni tulikuwa na shida sana maana wale viongozi tulikuwa nao Watanzania waliona ni kama tuko na vita. Sisi Wakenya ni watu wa amani. Chenye tunataka ni kufanya biashara pamoja maana Watanzania ni ndugu zetu na tunawapenda sana. Uhusiano usiwe tu na Watanzania peke yake. Tushikane pia na majirani wengine kama Uganda. Nashukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya kwani jana nilimuona Uganda katika sherehe ya kutawaza Rais Yoweri Museveni. Naomba Rais azidi kutembea ndio tuweze kufanya biashara pamoja. Inajulikana wazi kuwa ile biashara Wakenya wanafanya zaidi ni hapa sehemu zetu za Afrika Mashariki. Kama tungeruhusiwa tufanye biashara pamoja, haingekuwa haja ya kuenda mbali. Wananchi wa hili jimbo wako na uwezo wa kusaidiana na kuendeleza nchi zetu mbele. Si lazima wakati wote tunategemea watu wa ng’ambo. Nauliza Waafrika wajiheshimu na tuwe na mashirika yanayoweza kutusaidia. Kwa vile naona kuna wenzangu wanataka kuongea, niseme Kiswahili changu kimefika hapo. Nafikiri hata mimi nimepita Kiswahili. Asante."
}