GET /api/v0.1/hansard/entries/1072276/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072276,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072276/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilome, WDM-K",
    "speaker_title": "Hon. Thuddeus Nzambia",
    "speaker": {
        "id": 13375,
        "legal_name": "Thaddeus Kithua Nzambia",
        "slug": "thaddeus-kithua-nzambia"
    },
    "content": " Asante sana, Bi Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa hii fursa kuchangia huu mjadala muhimu. Kwanza nataka kushukuru Wabunge wote waliompokea Mhe. Rais Suluhu kwa shangwe na vigelegele. Hiyo ilimpa motisha sana ya kutupatia habari kamili kuhusu nchi zetu mbili. Nataka kushukuru Rais Uhuru Kenyatta kwa kuchukua nafasi ya haraka sana kumkaribisha mwenzaki jirani Rais Suluhu. Kwa muda tumekuwa na shida nyingi sana. Na hicho ni kitu cha kusema bila uwoga wala kuficha. Wanabiashara wa Kenya wamekuwa na shida ya kufanya biashara Tanzania. Kuwemo kwa Rais wa Tanzania hapa kwetu kulitupatia nafasi safi ili biashara iendelee na amani. Ushirikiano na umoja unaimarisha maendeleo katika nchi yoyote. Ule undugu Suluhu mwenyewe alituonyesha ilibainika wazi kwamba tukiendelea hivyo katika nchi hizi mbili, itakuwa ni kwa manufaa yetu sisi wote. Kuna kitu muhimu katika nchi jirani. Wakati kuna umoja, biashara na maendeleo huimirika haraka sana. Pia ningependa kushukuru Rais wetu Uhuru Kenyatta kwa kuchukua nafasi kumualika Rais Suluhu, kwa sababu moja: zile shida zimekuwa katika mipaka ya nchi zetu mbili, ilibainika wazi kwamba kumekuwa na uhuru wa kufanya biashara na kuimarisha maisha ya Wakenya na Watanzania. Pia, nachukua nafasi hii kushukuru ukarimu wa Rais Suluhu kwa kuitikia wito wa kututembelea. Kama walivyosema wenzangu, ilikuwa nafasi nzuri kwa viongozi wetu The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}