GET /api/v0.1/hansard/entries/1072279/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072279,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072279/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Isiolo North, KPP",
"speaker_title": "Hon. Hassan Hulufo",
"speaker": {
"id": 13348,
"legal_name": "Hassan Oda Hulufo",
"slug": "hassan-oda-hulufo-2"
},
"content": " Ahsante sana Naibu Spika wa Muda kwa hii nafasi. Ninaunga mkono hii Hoja ya Hotuba iliyotolewa katika Bunge hili na Rais Samia Suluhu wa Muungano wa Tanzania. Ujio wa Mhe. Rais Suluhu Hassan, kwa hakika, ulikuwa safari yake rasmi ya kwanza tangu alipochukua usukani wa wa nchi hiyo, na hiyo ni heshima kubwa kwa nchi yetu. Namshukuru Rais wetu pia. Rais Suluhu alituambia kwamba Mhe. Uhuru Kenyatta alikuwa kiongozi wa kwanza kuwafariji Watanzania alipopata habari ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli. Rais Suluhu pia alitueleza jinsi Rais Uhuru Kenyatta alivyokatiza hotuba yake kwa muda kwa heshima ya adhana ya kuwaita Waislamu kwenda msikitini kusuali alipokuwa akiwafariji Watanzania kule Dodoma. Hilo ni jambo lililowafanya Watanzania kumuona Rais wetu kama kiongozi anayethamini na kuiheshimu dini ya Kiislamu. Rais Suluhu ametuonyesha kuwa viongozi kina mama wako na hekima. Alikaa kwa kikao na Rais wetu na wengine wanaoendeleza Serikali yetu. Hiyo, ilimuwezesha kuelewa dhana tulizonazo kuhusu Tanzania; kama ile dhana ya kwamba Watanzia wanachukia Wakenya, na kadhalika. Rais Suluhu pia aligusia masuala yanayounganisha hizi nchi mbili jirani, na ni mengi kuliko yale ambayo hatukubaliani nayo. Kuhusu yale mambo machache ambayo hatukubaliani nayo, Rais Suluhu alisema kwamba hayaambatani na msingi wowote isipokuwa kile alichokiita"
}