GET /api/v0.1/hansard/entries/1072288/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072288,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072288/?format=api",
    "text_counter": 138,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Ruiru, JP",
    "speaker_title": "Hon. Simon King’ara",
    "speaker": {
        "id": 13468,
        "legal_name": "Simon Nganga Kingara",
        "slug": "simon-nganga-kingara-2"
    },
    "content": " Asante Sana, Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii nichangie mema na mazuri ambayo yanatuleta sote katika eneo la Afrika Mashariki. Mwaliko wa Rais wa Tanzania Bi. Samia Suluhu ulifanywa na kiongozi mwenye hekima, Rais Uhuru Muigai Kenyatta. Ninawapongeza wote wawili kwa kutumia njia hiyo kama nafasi ya kuleta uwiano katika maendeleo ya Afrika Mashariki. Kuna Nchi sita zinazoshirikiana katika Afrika Mashariki. Tukianza na Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuliko nyingine kwa ukubwa wa ardhi, ninaona maisha yakiwa mazuri. Alinivutia pia wakati marais wote wawili walipoangazia vile tutafungua mipaka yetu. Mipaka kati ya Kenya na Tanzani ni mingi. Mifano ni Namanga, Lunga Lunga, Isebania na Sirare. Wafanyabiashara wetu wamekuwa na shida sana katika shughuli zao za biashara pale katia mipaka. Viongozi hao walipokutana walijaribu kulainisha vile biashara inaweza kunoga kati ya nchi hizi mbili, na kuonyesha maendeleo yatapatikana. Pia, waliongea kuhusu usalama. Hapa kwetu, tumekuwa na shida ya usalama hapa na pale. Nchi zote mbili zikiungana, na haswa zikileta nchi nyingine kwenye muungano huu, hali ya usalama itakuwa nzuri. Akigusia masuala ya utalii katika nchi zote mbili, Rais Suluhu alisema kwamba kulikuwa na changamoto kwa vile Wakenya na Watanzania hawakuwa wakifanya biashara bila ya matatizo katika maeneo ya hifadhi za wanyamapori za Serengeti upande wa Tanzania na Maasai Mara upande wa Kenya…"
}