GET /api/v0.1/hansard/entries/1072289/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072289,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072289/?format=api",
    "text_counter": 139,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Starehe, JP",
    "speaker_title": "Hon. Charles Njagua",
    "speaker": {
        "id": 13283,
        "legal_name": "Charles Kanyi Njagua",
        "slug": "charles-kanyi-njagua"
    },
    "content": " Asante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia hotuba ya Rais wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu. Kwanza kabisa ni kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Kenya na Rais wa Tanzania kwa kushikana na kuonelea ni vizuri wakutane na wafanye kazi pamoja. Mwaka uliopita nilitamka matamshi ambayo yalileta shida sana katika nchi hii na nchi jirani. Na mimi kama Mbunge wa Starehe nilikuwa natetea wale wakaaji wa Starehe ambao wengi ni wafanyabiashara. Kumekuwa na changamoto nyingi sana na mimi nilifurahia sana wakati Mhe. Suluhu, Rais wa Tanzania, alipozuru nchi yetu kwa sababu ilionyesha kwa kweli kulikuwa na matatizo ambayo nilikuwa nimeyaongea. Na mimi nataka niseme ni kitu cha maana sana sisi kufanya kazi pamoja na Tanzania. Tumekuwa na tulikuwa na shida nyingi sana kama vile Waheshimiwa wengine wamesema, kwa maneno ya kilimo na maneno ya wafanyabiashara. Ulikuwa unapata mfanyabiashara akitoka hapa akienda nchi Jirani, kuna mahali hangeweza kufanyia biashara; kuna mahali angewezaenda na asiingie. Wengine wananunua mizigo wakiwa juu ya miti lakini wale Watanzania wakija Kenya unapata wanafanya biashara bila kusumbuliwa. Kwa hivyo, nikimalizia kwa sababu sitaki kupoteza muda sana, nataka niwaeleze wale waliopatiwa majukumu na marais hao wawili kulainisha biashara za hizi nchi mbili, wakae chini, sio na matajiri pekee, wakae chini na hata wakulima wadogo wanaoteseka wakati nchi hizo mbili zinazozana. Asante sana. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}