GET /api/v0.1/hansard/entries/1072357/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072357,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072357/?format=api",
    "text_counter": 24,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "kuzorota kwa huduma za mahakama wakati huu wa janga la Korona yaani (COVID-19). Malalamiko haya yamekuja wakati mwafaka kwa sababu tumeona kwamba huduma za mahakama zimeendelea kupungua kwa sababu ya janga la Korona lililotekea Mwezi wa Tatu mwaka jana. Kumekuwa na kufungwa kwa mahakama mara kwa mara kwa sababu mmoja au wawili wa wafanyikazi wa mahakama wameweza kupatikana na ugonjwa wa Korona au COVID-19. Kwa hivyo, si salama kwa watumizi na wahudumu wa mahakama kuendelea kufanya kazi wakati wenzao wamepatikana na janga hilo. Bw. Spika wa Muda, athari zaidi zimewapata mawakili kwa sababu wengi wao hutegemea huduma za mahakama ili waweze kukidhi mahitaji yao na kusimamia ofisi zao. Wengi wameweza kuathirika na kufunga ofisi zao kwa sababu kazi zimepungua, na vile vile, huduma katika mahakama zimeendelea kupungua. Kumeongezeka msongamano katika jela zetu kwa sababu wengi wa wale ambao wanapewa masharti ya kutoka nje wakati wanangojea kesi wanashindwa kuyatekeleza kwa sababu ya hali ngumu ya uchumi kutokana na janga hili la COVID-19. Kwa hivyo, nakubaliana na mawazo yaliyotolewa na Sen. Cheruiyot kwamba swala la pesa zinazoenda kwa taasisi ya mahakama lazima ziongezwe, kwa sababu wataweza kuhudumia wananchi kwa urahisi zaidi iwapo watakuwa na pesa za kutosha. Bw. Spika wa Muda, awali ilipotokea janga la COVID-19, mahakama nyingi hazikuwa na hazina ya pesa za kuweka sehemu za kuosha mikono ama kununua viyeyuzi na kupeana barakoa kwa wale ambao labda wameingia mahakamani na hawakuweza kuwa na barakoa, na wale ambao labda zao zimeharibika wakiwa mahakamani. Swala la pesa kwa mahakama ni muhimu sana. Hii ni kwa sababu bila pesa imekuwa ni mambo ya mshike mshike katika mahakama zetu nchini Kenya. Swala lingine ni kuwa huduma za kimtandao katika mahakama mara nyingi huwa zimedorora. Utapata kwamba mawakili wanaingia katika mtandao Saa Tatu lakini inawachukua masaa mawili ndio majaji waweze kuingia. Ukiuliza unaambiwa mtandao ulikuwa uko chini, kwa hivyo hatuwezi kuanza vikao vya korti. Bw. Spika wa Muda, mara nyingi utapata kwamba mawakili wanapiga kelele na kuuliza: “Je, unanisikiza mheshimiwa? Can you hear me your Honour?” Muda mwingi unapotea wakati hawawezi kuelewana baina ya yule wakili ama mhusika na yule anasimamia korti ile. Ikiwa mahakama zetu zitapewa pesa za kutosha, zitasaidia kuimarisha miundo msingi ya mitandao yake. Hii ni kwa sababu bila miundo msingi dhabiti mara nyingi wakati unapotea katika vikao vya mahakama. Mahakama siku hizi zimefungua ile inaitwa e-filing, lakini ukijaribu kuingia kwenye mtandao unaambiwa uko chini. Ukirudi tena Saa Nane, unaambiwa bado mtandao uko chini. Baadaye mtandao unapoimarika unaambiwa sasa kuna msongamano kwa sababu kuna watu wengi ambao wanajaribu kuingia kuweza kusajilisha hati zao, lakini mtandao hauwezi kusaidia. Bw. Spika wa Muda, inamaanisha kwamba kuna kuchelewa kuwasilisha kesi mahakamani. Kuna kuchelewa kuweza kulipa malipo kwa mahakama. Kuna kuchelewa kuweza kutekeleza yale ambayo yanatakikana yatekelezwe kabla hukumu haijatolewa ama masharti hayajatoka. Kwa mfano, kama kesi inataka kupelekwa kwa haraka, yaani ile wanaita certificate of urgency, mara nyingi inakuwa ni shida. Inakuchukua karibu siku"
}