GET /api/v0.1/hansard/entries/1072359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072359,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072359/?format=api",
    "text_counter": 26,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "tatu kama wakili kuweza kuhakikisha kwamba maombi yako yamefika mbele ya mahakama ili yaweze kushughulikiwa. Hili swala la ufadhili ni muhimu. Pia swala la kuongeze mahakama nchini ni muhimu. Mahakima zetu ni chache na huchangia misongamano. Ninaunga mkono malalamiko haya ambayo yameletwa katika Bunge letu la Seneti. Ningeomba swala hili lishughulikiwe na Kamati yetu ya Haki na Maswala ya Kisheria na Kamati ya Bunge ya Kitaifa ili kuhakikisha kwamba yameweza kutekelezwa. Bw. Spika wa Muda, mwisho ni kuwa katika maswala ya mtandao wengi hawapati fursa ya kuweza kuelezewa mashtaka kwa lugha wanazozifahamu au wanaotakikana kufuatilia kwa urahisi. Kwa mfano, hatujakuwa na mtandao unaotumia lugha ya Kiswahili ama lugha nyingine ambazo zinatumika mahakamani kama zile sehemu za mashambani ambazo inakuwa ni rahisi kwa mtu kuweza kufuatilia kesi yake. Itakapotafsiriwa kwa mfano kwa Kiswahili, itakuwa inasaidia pakubwa kwa yule ambaye anasomewa mashataka. Nachukua fursa hii kumpongeza hakimu mmoja katika mahakama ya Shanzu ambaye majuzi aliandika na kusoma hukumu yake kwa lugha ya Kiswahili kuanzia mwanzo hadi mwisho. Hakimu huyo anaitwa Senior Resident Magistrate Odhiambo ambaye anahudumu katika Mahakama ya Shanzu kule Mombasa. Bw. Spika wa Muda, hii inamaanisha kwamba lugha ya Kiswahili inaendelea kukua na iwapo tutaweza kupata nafasi ya kuajiri wakalimani wa kutosha, itakuwa ni lugha ambayo inatumika vizuri mahakamani bila tashwishi yoyote. Hiyo itasaidia popote kutekeleza swala la upatikanaji wa haki kwa sababu anayesomewa mashtaka atayaelewa. Yule anayesomewa hukumu ameelewa hukumu ile ili asitendewe visivyo katika mahakama ile ambaye inahusika. Kwa hivyo, ninaunga mkono malalamiko hayo. Bw. Spika wa Muda, asante."
}