GET /api/v0.1/hansard/entries/1072375/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072375,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072375/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Ulegevu wa huduma za sheria katika hizi korti umekithiri. Yote haya yanaletwa na hili janga la homa ya korona au COVID-19. Hususan, mawakili wanapata shida kutafuta tarehe ya kesi zao kusikizwa kupitia kwa matandao. Sio kama zamani ambapo mawakili wangeenda kortini, kuorodhesha kesi na kutetea wateja wao mara moja. Wakati huu, kesi zinalegea na haki za wananchi kucheleweshwa. Kama tunavyojua, ikiwa haki itadidimia kwa mwananchi, ni sawa na kusema mwananchi amenyimwa haki. Kumnyima mwananchi haki yake ni makosa. Katika Kaunti ya Kilifi, kesi za mashamba ndizo zinachelewa zaidi. Imekuwa vigumu sasa kwa watu kuwania na kuzuia cheti cha dharura. Sasa unapata mabwanyenye wanatumia hilo kama kinga yao. Mara kwa mara wananapata amri na wanavunja mahali ilhali wakili wa ule upande mwingine akitaka kwenda kortini kutumia cheti cha dharura, anapata kwamba hawezi kufikia korti. Kunatakiwa kuwe na mageuzi na kuweka njia rahisi kupitia kwa mtandao ili hawa mawakili wawasilishe maswala ya dharura kama haya. Bw. Spika wa Muda, watu wengi wanapata taabu. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Serikali imeendelea kupunguza pesa za mahakama. Tunahitaji mahakama kila mahali ili watu wasisafiri kwenda mbali kutafuta haki. Hebu fikiria kutoka Mtwapa hadi Malindi ikiwa kesi iko kule. Inabidi maskini achukue pesa zake za matumizi ili asafiri. Kuna haja ya Serikali kutenga pesa za kutosha ili mahakama za taifa ziimarishe mitandao yao kwa ajili ya mawakili kufanya kazi bila matatizo katika huduma kwa wananchi."
}