GET /api/v0.1/hansard/entries/107239/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 107239,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/107239/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mung’aro",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 76,
        "legal_name": "Gideon Mung'aro Maitha",
        "slug": "gideon-maitha"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, ningependa kusimama niulize taarifa kutoka kwa Waziri wa Utawala wa Mikoa na Usalama wa Ndani. Mnamo asubuhi ya 31st March, 2010, kikosi cha polisi na Askari wa Utawala kilivamia maskwota Watamu katika eneo Bunge la Malindi katika oparesheni ambayo ilikusudiwa kuwafurusha maskwota hao katika kipande cha ardhi kilichokuwa kikizozaniwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na mfanyibiashara mmoja wa Watamu. Katika uvamizi huu, vijana wawili walifariki na kadhaa kupata majeraha mabaya ya risasi. Kufuatia tukio hilo, ningeliomba Waziri mhusika kueleza ni katika mazingara gani yaliopelekea polisi kuvamia kipande hiki cha ardhi usiku wa manane kikiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani? Pili, ni watu wangapi walijeruhiwa mikononi mwa polisi katika mkasa huu na kwa hivi sasa wako katika zahanati gani na hali yao ya kiafya ikoaje? Tatu, ni hatua gani Waziri amechukua kwa Mkuu wa Mkoa huo kutokana na kitendo hiki cha kinyama kwa watu wa eneo la Ubunge la Malindi? Na mwisho, ni hatua gani Waziri anakusudia kuchukua dhidi ya askari polisi na wa utawala waliohusika katika mauaji hayo?"
}