GET /api/v0.1/hansard/entries/1072429/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072429,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072429/?format=api",
"text_counter": 96,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwanza kabisa nachukua fursa hii kukushukuru kwa kunipa fursa ya kuchangia ombi hili ambalo limeletwa na Maolo Kiprotich kuhusiana na kuhamishwa na kupokonywa ardhi kwa jamii ya Torobeek ambayo iko katika maeneo ya Nandi. Jambo hili ni dhuluma za kihistoria ambazo zimefanywa na Waingereza, sio hapa Kenya pekee yake lakini sehemu nyingi ulimwenguni. Hivi tunavyozungumza, kuna dhuluma kama hizi zinazoendelea kule Palestine ambapo Serikali ya Israeli inawahamisha kwa lazima Wapalestina kutoka ardhi zao za jadi. Hii sio suala geni ulimwenguni. Ni suala ambalo limekuwepo katika vichwa vya habari kwa miaka mingi lakini jambo la kusikitisha ni kwamba taasisi zote za ulimwengu zimekaa kimya wakati Wapalestina wanadhulumiwa haki zao za jadi. Tusiwaangalie ni kama ni Waarabu wa Palestina; tuwaangalie kama binadamu, kwamba wao wana haki kama binadamu wengine. Wana haki za kuishi kwa amani kama watu wengine wote. Kwa hivyo, tunavozungumzia swala hili la Turbi ni lazima tuangazie zile dhuluma za kihistoria ambazo zimefanywa na wabeberu wakati wa nyuma na sasa zinafanywa na wananchi wenyewe wa Kenya katika Serikali yao ya Kenya. Juzi kulikuwepo na eviction kama hii kule mjini Mombasa kati ya mpaka wa Mombasa na Kwale County. Yaliofanyika pale yalikuwa mambo ya dhuluma kabisa kwa sababu watu walivamiwa usiku wa manane. Nyumba zao zilivunjwa bila wao kuonyeshwa court order. Watu walikuja na kuvunja nyumba zao kama vile wanavyofanyiwa Palestina, Gaza na kwingineko. Swala hili limekuwa donda sugu katika nchi yetu. Tumezungumzia hapo nyuma swala la eviction katika sehemu ya Baba Dogo hapa Nairobi, eneo ya Diani na sehemu za Kilifi. Katika sehemu hizi zote, evictions zinafanyika usiku wa manane. Kuna suala la curfew. Itakuwaje polisi wakavamie watu usiku wa manane wakati kuna curfew? Je, hii curfew ni ya wale ambao wanazunguka barabarani pekee yake? Wale wanaokuja kuvunjia watu nyumba usiku, hawaadhiriwi na curfew? Ningeomba suala hili lipewe Kamati ya Sheria kwa sababu hii mambo inahusu sheria ya kumiliki ardhi, sheria ya kumiliki nyumba, sheria ya kuhamishwa kiholela kinyume na haki za binadamu na zile haki zingine za kimataifa. Naomba kamati ambayo itashughulikia swala hili iangalie kwa undani zaidi kwa sababu ni swala ambalo linaadhiri mpaka sasa; sio zile dhuluma za zamanbi. Mpaka sasa, dhuluma hizi zinaendelea katika nchi yetu. Bw. Spika wa Muda, ninaunga mkono."
}