GET /api/v0.1/hansard/entries/1072456/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072456,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072456/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Bwana Spika wa Muda. Kwanza ninampongeza huyu Paulo Kiprotich. Hali wanayoipitia watu hawa wa Torobeek si nzuri. Kwa mara nyingi tumekuwa tukiona Wakenya wanagawanyana kwa sababu ya msingi kama huu. Si haki ikiwa kila mtu hapa anaishi kama Mkenya kuweza kudharau Wakenya wengine. Ninasema hivi kwa sababu hawa kama alivyosema Sen. Cherargei, pia ni Wakenya. Wanatakikana kutambuliwa na serikali na sheria. Tunajua kuna wale watu wanaitwa Wadorobo ambao wanaishi huko kwenye milima na misitu. Lakini katika miaka na vikaka, hao hawajaharibu ule msitu. Ikizidi zaidi wanautunza. Ni jambo la aibu hivi leo kuona ya kwamba ni Serikali yenyewe ndio inahusika na kuenda kuwachukua hawa Watorobeek na kuwafukuza katika hizi nyumba ambazo wamekuwa wakiishi. Mara nyingi tunaona inafanywa katika hali ya ukosefu wa haki za binadamu. Hili ni jambo la kusikitisha hususan likifanywa na maafisa wa Serikali ambao wanajua kabisa vile wanafanya sio utendaji haki."
}