GET /api/v0.1/hansard/entries/1072457/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072457,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072457/?format=api",
"text_counter": 124,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, ardhi ni kitu muhimu sana katika nchi yetu ya Kenya. Watu wengi wamekuwa wakitengeneza hati milki bandia. Kama kuna zile tunaita stakabadhi za bandia, ziko nyingi sana kupita kiasi ndani ya Kaunti ya Kilifi. Watu wengi sana wamepata taabu kuweza kufurushwa katika mashamba yao kwa sababu mtu amekuja na cheti. Watu wameishi hapo zaidi ya miaka arobaini ama sabini. Watoto wamesoma, mababu wamekufa na wamezikwa hapo. Kila mtu amezikwa hapo na kuna makanisa na shule watu wanaenda."
}