GET /api/v0.1/hansard/entries/107259/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 107259,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/107259/?format=api",
    "text_counter": 255,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Joho",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 30,
        "legal_name": "Hassan Ali Joho",
        "slug": "hassan-joho"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, mtu anayetajwa kuhusika katika jambo hili ambalo limeleta maafa ya watu wawili na watu kumi kujeruhiwa kwa risasi ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani ambaye yuko afisini mpaka sasa. Bw. Waziri Msaidizi yeye amesema alizuru eneo hilo na lilikuwa sawa. Mimi nilikuwa huko Jumamosi na hali ni ya taharuki. Ni hatua gani itakayochukuliwa mara moja ili uchunguzi wa haki ufanywe?"
}