GET /api/v0.1/hansard/entries/1072745/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072745,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072745/?format=api",
    "text_counter": 228,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Gavana wa Kaunti ya Wajir pia alishtakiwa kwa kosa la kukiuka vifungu 176(i) na 185 vya katiba. Maelezo ni kuwa Gavana alipuuza Bunge la Kaunti la Wajir katika kupeleka rasilmali zinazofaa katika bunge hilo la kaunti. Ni wazi kwamba PublicFinance Management (PFM) Act, 2012 inasema kwamba fedha za serikali ya kaunti na fedha za bunge la kaunti zinafaa kuwekwa tofauti lakini kufikia sasa, mabunge mengi ya kaunti yanategemea ruzuku kutoka serikali za kaunti. Fedha hizo hutolewa siku ambayo gavana au waziri wa fedha wa kaunti ile anapopenda. Nilihudumu katika kamati ya uhasibu la bunge hili. Tulishuhudia tukio hilo katika kaunti nyingi na sio maajabu swala hilo linaendelea. Mara nyingi, mabunge ya kaunti yanashindwa kutekeleza majukumu yao wakati pesa zimezuiliwa na serikali za kaunti wakati pesa hizo vinapaswa kutolewa kwa wakati unaofaa."
}