GET /api/v0.1/hansard/entries/1072749/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072749,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072749/?format=api",
"text_counter": 232,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Shtaka lingine dhidi ya Gavana huyu ni kuwa alikosa kutoa taarifa rasmi kwa Bunge la Kaunti ya Wajir kupitia county address . Hiyo ni moja kati ya mambo muhimu kwa sababu ile hotuba gavana anayotoa kwa bunge la kaunti, Gavana hutoa mwongozo wa mambo anayotarajia kufanya katika mwaka ule. Ni muhimu kwa magavana kutoa hotuba hiyo ili kuhakikisha kwamba wabunge wote wa bunge la kaunti wana uelewano kwamba sheria zote zitakazoletwa katika bunge lao mwaka ule zitakuwa za mtazamo gani. Swala hilo pia halikuweza kuthibitishwa na Kamati Teule."
}