GET /api/v0.1/hansard/entries/1072753/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072753,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072753/?format=api",
    "text_counter": 236,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bw. Spika, tumesema mara kwa mara katika bunge hili kwamba afya ni huduma muhimu ambayo inafaa kutolewa kwa usawa kwa wananchi katika kaunti zetu. Kumekuwa na ubadhirifu wa fedha za COVID-19 takriban kaunti zote 47 katika Jamhuri yetu ya Kenya. Tumeona kwamba ukosefu wa huduma za afya hususan katika kaunti zilizo mbali na miji mikuu kama kaunti ya Wajir ilioko mbali na miji mikuu. Wakaazi wa Kauti ya Wajir hulazimika kusafiri kwa muda mrefu ili waweze kupata hudum za afya ikilinganishwa na kaunti za mjini kama Nairobi, Mombasa na Kisumu."
}