GET /api/v0.1/hansard/entries/1072754/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072754,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072754/?format=api",
"text_counter": 237,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, swala kuu ni kwamba, je, hili swala hilo moja lilothibitishwa, laweza kumpata gavana wa Kaunti ya Wajir na hatia ya kumwondoa mamlakani? Ndio, kwa sababu Gavana hakuweza kutekeleza majukumu yake kulingana na sheria ambayo imewekwa nchini. Maseneta wengine wamejadili kwamba makosa kama hayo yapo pia katika serikali ya kitaifa. Seneta wa Nandi alisema kwamba hata Mhe. Mutahi Kagwe, Waziri wa Afya katika Serikali ya Kitaifa pia anafaa kutolewa ofisini lakini swala ni kwamba hata yeye anaweza kuleta hoja hapa bungeni na ikithibitishwa, pia Mhe. Kagwe ataenda nyumbani."
}