GET /api/v0.1/hansard/entries/1072937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1072937,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072937/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Spika. Ningepemda kujiunga na stetimenti hii ambayo imeletwa na ndugu yangu, Sen. Mohamed Faki wa Mombasa. Kama tunavyoelewa, Kenya iko katika radar au map ya ulimwengu. Matumaini yangu ni kwamba watu wengi sana katika Kenya, hususani wakiwa ni wakrsito, wameweza kwenda kule. Hii ni kwa maana ile ndio kama maka yao kwenda kuona pale Yesu alizaliwa, makalio yake, na aliishi vipi pande hizo zote za Jerusalem. Tunaona kwamba, kukiwa na uhusiano bora katika yale maeneo baana ya Waisreaeli and Filistini huenda kukawa na Amani na maendeleo. Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba Israeli hivi leo inachukuwa mkondo ambao sio wa kibinadamu. Israeli wanaweza kulipua bomu kule. Basi wapeleke hayo mabomu yao kwa upande kuna vita. Wale wengine watarejesha hayo mabomu vile vile kama wanavyoelewa. Mabomu haya yanaelekezwa katika nyumba na maeneo ambayo yako na watu wengi kama mahospitali, maduka; watu ambao hawahusiki kabisa na tofauti zao kijeshi. Kwa miaka mingi, watu walikuwa wakipigana baina ya Israeli na Palestina. Lakini baada ya Arafat kuja, yule aliyekuwa mkubwa wa Palestina aliweza kuzungumza kwa kina na watu wa Israeli. Hatimaye ukikumbuka historia ni kwamba amani ilipatikana. Wakati wao watu wengi hawakufariki ama hapakutokea shida tena baina ya Israeli na Wafilisti."
}