GET /api/v0.1/hansard/entries/1072939/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1072939,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1072939/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Lakini tunaona ya kwamba baada ya yeye kuondoka wale waliochukua utawala katika upande wa Israeli ikiwamo huyo Waziri Mkuu aliyepo sasa, haiandamani na yale mambo ambayo yaliwekwa ya amani wakati ule. Kwa hivyo, hata kama Yasser Arafat alikiuka haki za watu, wale walioko kama viongozi ni muhimu waweze kukaa, kuongea na kuona ya kwamba kila wakati wanapotumia zile zana zao za vita wanaokufa ni raia sio wanajeshi. Hii ni kwa sababu wanajeshi wanajua mbinu za kujitetea. Hii hasara ambayo Israeli inapeleka saa zote kwa Wapalestina ikome. Kama alivyosema ndugu yangu Sakaja sisi tunaketi katika kile kitengo cha juu sana katika usalama wa nchi za United Nations. Ikiwa tunaketi katika ile meza ya kuangalia amani itakuwa jambo la aibu ikiwa Kenya haitatoa matamko ambayo yanakemea vile watu wanavyokufa kule Palestina. Bw. Spika, tunaelewa kwamba kila mwaka kunakuwepo na mwezi mtukufu wa Ramadhan. Wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kila mtu anataka amani kwa sababu huu ni wakati wa kuzingatia akili zetu ziwe mbele ya maombi na kujiweka mbele ya Mwenyezi Mungu. Lakini utapata kwamba Waisraeli wako katika mstari wa mbele wakati wa amani kama huu ambapo inatakikana kuwe na amani ulimwenguni na watu wanafunga kwa sababu ni mwezi mtukufu. Kila mtu anaelekeza uso wake na fikira zake kwa Mwenyezi Mungu na kuomba kwamba amani iweze kupatikana katika nchi ni makossa sana kwa Israeli wale upande ule wa Palestina na mabomu na kuua watu. Wakati mwingi tunaona kwenye runinga akina mama wakikimbia na watoto wadogo kabisa. Tunaona wakipelekwa mahospitali. Katika hizo harakati tunaona mara nyingi Wapalestina wengi ndio wanaokufa. Huu ni wakati wa Kenya kuweza kujitambulisha katika mataifa ya ulimwengu ya kwamba wanakemea vikali tabia za Israeli kuua wenzao wanaoishi pamoja. Tunajua mipaka ya Israeli na mipaka ya Palestina haitageuka hata kidogo milele na milele. Kwa hivyo, ni lazima hawa watu waanze kuzoeana, kujuana na kupendana ili amani ipatikane katika hii mipaka yao. Bw. Spika, ninaunga mkono."
}