GET /api/v0.1/hansard/entries/1073009/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073009,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073009/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": "Wiki iliyopita, rafiki yangu ambaye ni mwanahabari tajika anayefanya kazi katiza Kituo cha Televisheni cha Citizen, Bw. Rashid Abdalla, alinihimza sana. Aliniambia kwamba kila tunapozungumza, mimi hutumia Lugha ya Kiwsahili, lakini mbona hajawahi kuniona nikizungumza katika Kiswahili huku Bungeni ilhali nimesoma? Katika shule ya msingi, nilisoma Lugha ya Kiswahili kwa miaka minane. Baada ya hapo, nilienda shule ya upili na kujifunza Kiswahili miaka minne mengine. Sasa nimekuwa Bungeni karibu miaka saba, lakini sijawahi kuzungumza katika Kiswahili. Nilisema kwamba nitajikaza kuzungumza katika Kiswahili tutakapojadili Hotuba ya Rais Suluhu Hassan. Nitapeana mawazo yangu kuhusu jambo hili ili nijihisi kama niko miongoni mwa wale wanajumuika katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Inasemekana kuwa tusiwe tu watu wa kujumuika kwa sababu Mwenyezi Mungu amesema tuishi pamoja, lakini tujaribu kuwiana kupitia lugha yetu na tuzungumze lugha ambazo tunaelewana. Bw. Spika, sifikiri kama kuna lugha nyingine yoyote ambayo inaeleweka sana katika Jumuia ya Afrika Mashariki kuliko Kiswahili. Kwa hivyo, nitajikaza niseme mambo haya."
}