GET /api/v0.1/hansard/entries/1073012/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073012,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073012/?format=api",
    "text_counter": 186,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, kabla sijaanza ningependa kusema jambo fulani. Bi. Spika wa Muda, yamkini mwaka mmoja umepita tangu Bunge la Kitaifa kukubaliana kuzungumza Kiswahili kila Ijumaa. Iwapo wewe hufuatilia mazungumzo yao katika runinga, mara nyingi, Wabunge huko hujikaza. Sio kwamba ati wanaelewa Kiswahili sana ama lugha yao ni nzuri zaidi lakini ni tabia ambayo watu wanajifunza. Kidogo ninaona hata rafiki zangu ambao katika hali yao, hawaelewi hii lugha sana lakini sasa wamejifunza hadi wanaweza kuzungumza."
}