GET /api/v0.1/hansard/entries/1073014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073014,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073014/?format=api",
"text_counter": 188,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13165,
"legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
"slug": "aaron-cheruiyot"
},
"content": "Bi Spika wa Muda, wacha niseme mawili au matatu ambayo nilijifunza kutoka kwa Hotuba ya Rais Suluhu Hassan, majuma mawili yaliyopita. Bado ninakumbuka mambo hayo vizuri sana na pia ninafikiria wakati wowote ninapofikiria kuhusu uhusiano kati ya Kenya na Tanzania. Tanzania imebarikiwa na viongozi wa kike ambao wanaendesha uongozi wao kwa njia inayofurahisha. Iwapo wewe hufuatilia maswala ya Bunge la Tanzania na uongozi, utanielewa. Kuna viongozi watatu wa kike ambao mimi huwafuatilia sana uongozi wao na yale wanayofanya."
}