GET /api/v0.1/hansard/entries/1073018/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073018,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073018/?format=api",
"text_counter": 192,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13165,
"legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
"slug": "aaron-cheruiyot"
},
"content": "Kiongozi wa tatu wa kike ambaye nilikuwa nikimfuatilia tangu akiwa Naibu wa Rais, ni huyu Mama, Samia Suluhu Hassan. Sijui kwa nini lakini ninaona mambo mengi aliyosema katika Hotuba yake hayakuwa mageni. Sio mambo ambayo hatujawahi kuzungumzia hapa Bungeni au kuyasikia kutoka kwa viongozi wengine. Hata hivyo, alizungumza kwa sauti yake ya upole na ustaarabu, alichukua nafasi yake na kutueleza huku akisita ili kuhakikisha tunamwelewa. Mambo hayo yamebaki akilini mwangu na kwa Wakenya wengi. Iwapo unafuata mazungumzo ya Wakenya katika maeneo ya burudani au hata mitandao ya kijamii, utaona Wakenya wengi wameelewa umuhimu wa kuwa na uhusiano mwema kati ya nchi hizi jirani. Mhe. Rais alitukumbusha kwamba Mwenyezi Mungu hakukosa kutuweka pamoja katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Alisema kwamba kuna watu wenye fikira potovu nchini Tanzania na pia Kenya, watu wanaofikiria wanaweza kunawiri peke yao bila wenzao. Alituhimiza tuwache mawazo kama hayo na kwamba ili haya mataifa jirani kustawi zaidi, ni muhimu kutembea pamoja na kusaidiana. Aliongeza kusema kwamba Watanzania wanaweza kutusaidia katika mambo tunayopambana nayo humu nchini. Vile, kuna mambo ambayo Watanzania wanaweza kujifunza kutoka kwetu. Hilo ni himizo nzuri sana. Rais Suluhu alieleza jambo moja ambalo hata mimi sikujua. Alisema ati tunaona uchumi wetu ni mdogo sana lakini Kenya inaorodheshwa katika nafasi ya tano kwa mataifa yanayowekeza sana nchini Tanzania. Hata hivyo, hatuchukui hiyo nafasi ya tano kwa sababu ya kushindwa na wengine. Mataifa tunayoshindana nayo yameendelea sana na yana utajiri mwingi. Alitaja Marekani, Uingereza, China, India na hatimaye Kenya. Mhe. Bi Suluhu alieleza kwamba kuna viongozi wasiochunga matamshi yao. Unakumbuka miaka miwili au mitatu iliyopita, Mbunge mmoja alisema maneno ambayo hayafai kutoka katika mdomo wa kiongozi. Aliomba msamaha baadaye na kusema hakuwa amefikiria vyema. Alikuwa ameamuru Watanzania waondoke Kenya. Ni vizuri kwamba viongozi katika Wizara ya Maswala ya Kigeni walitoa taarifa chini ya masaa mawili. Wakati huo, sikuelewa kwa nini mambo hayo yalikuwa yanafanyika kwa haraka hivyo. Ziara ya Rais Suluhu na Hotuba yake imenipa fursa ya kuelewa uhusiano wetu na Tanzania ni muhimu sana. Tanzania ni nchi tunayopaswa kuheshimu kwa sababu hata nao wametualika kwao kufanya biashara. Pia wafanyibiashara wengi hapa Kenya wanafanya biashara huko Tanzania. Niko na uhakika hawawezi kuwa wanafanya biashara huko bila faida. Kwa hivyo, sisi kama Waafrika, ni vizuri kuheshimu na kuishi vizuri na yeyote aliyekualika kwake na ukanawiri. Ninamshukuru Mhe. Rais kwa kututembelea na kutupatia taswira ambayo Wakenya wengi hatukuwa nayo. Ni kwamba hizi nchi mbili zinapozidi kushikana na kujenga uhusiano wa maana na tuwe na mtazamo wa kuinuana, tunaweza kufaulu hata zaidi badala ya mabishano na kutopendena. Kuna jambo la pili ambalo lilinufurahisha lakini sio kutokana na Hotuba yake. Ukisoma mawazo ya Rais huyu na vile anachukulia mambo, yeye sio mtu wa kupenda"
}