GET /api/v0.1/hansard/entries/1073020/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073020,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073020/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": "ubishi. Ni msomi. Mkiwa na tofauti za kimawazo, anaamini akupe nafasi useme yako kisha na wewe umsikize na hatimaye mkubaliane. Sijui nitakuwa nimekosea nikisema hili lakini jambo hilo lilifanya nikafikiria tungekuwa na viongozi wengi wa kike hapa barani Afrika, pengine tungekuwa mbele zaidi, kinyume na sisi wanaume tulio uongozini. Sisi wanaume tunaamini kama hukubaliani na mawazo yangu, basi tupigane, turushiane cheche za maneno ili nikuonyeshe jinsi niko na nguvu. Hayo hayakuwa mawazo ya Rais Suluhu."
}