GET /api/v0.1/hansard/entries/1073022/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1073022,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073022/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13165,
"legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
"slug": "aaron-cheruiyot"
},
"content": "Mimi nimepata nafasi kumfuatilia hata akiwa kule nyumbani kwao. Nakumbuka wakati mmoja alikuwa anazungumuza na wafanyikazi wa serikali wanaofanya kazi katika Tanzania Revenue Authority (TRA), kitengo chao cha kukusanya ushuru. Alikuwa anawazungumzia akiwaelezea kuhusu uhusiano kati yao na wafanyibiashara. Hapa nchini Kenya, Bi. Spika wa Muda, unajua kama kuna jambo ambalo wafanyibiashara wanaogopa na pahali wanateswa zaidi ni katika ofisi za Kenya Revenue Authority (KRA), wale ambao wanakusanya ushuru nchini. Mara nyingi, watu wengi hawapendi kuenda kule. Nakumbuka wakati mmoja nikiangalia Rais Suluhu Hassan akizungumza na wale akiwaeleza, “Tafadhalini, kama mna jambo ambalo mmetofautiana na mfanyibiashara yeyote, hakikisha kwamba mmekaa chini mkaelewana. Msiwe tu wenye haraka ya kufunga biashara za watu.” Hapa Kenya, wakati mwingine hata bila ya kuelezwa wakikutumia barua pepe ya kwanza na ya pili, ya tatu jambo ambalo utajua ni kupata akaunti zako za benki zimefungwa. Yeye alikuwa anawaeleza kuwa si hivyo. Aliwahimiza watembelee ofisi za wafanyibiashara hao na kuelewana ili nao kama kuna pesa fulani mnawadai, fanyeni hesabu ya pamoja na mkubaliane vile hao watalipa. Ukiangalia yale mawazo ambayo alikuwa anapeana katika shida ambazo huwa zinatokea mara nyingi kati yetu na Tanzania, wewe wajua wale madereva wanaoenda masafa marefu wanapofika Namanga, mara nyingi huwa tuna shida kati yetu na jirani zetu. Mimi nilisikia yeye akizungumza akisema, “Jameni, haya ni mambo sisi twaweza kuzungumza na kuelewana. Si mambo magumu.” Mara nyingi nimesikia viongozi kutoka upande ule na viongozi kutoka huku kwetu wakisema mambo ambayo hayasaidii katika mgogoro huu. Kwa hivyo, namshukuru sana. Bi. Spika wa Muda, nikikaribia kumalizia, najipa kongole sana. Sikuwa na imani kwamba ninaweza kuzungumza Kiswahili mpaka hii taa iwake. Nilifikiri baada ya dakika tatu nitapotea hapo lakini naona karibu masaa yanakwisha. Kwa hivyo, nafikiri nitakuwa ninafanya jambo hili. Nashukuru rafiki yangu aliye nihimiza kwamba nitie bidii na nizungumze kwa Kiswahili. Bi. Spika wa Muda, nitamalizia nikizungumza kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nilifurahishwa sana na mapendekezo na mawazo ambayo yule Rais wa Jamhuri ya Tanzania alitoa alipokuwa akizingumzia. Kwa mfano, ukitembelea mbuga"
}