GET /api/v0.1/hansard/entries/1073026/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073026,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073026/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Cheruiyot",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13165,
        "legal_name": "Aaron Kipkirui Cheruiyot",
        "slug": "aaron-cheruiyot"
    },
    "content": "unampa mtalii yeyote ambaye yuko sehemu zingine za duniani yaweza kuwa bora zaidi ukimuuzia ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuliko ukimuuzia ya nchi tofauti kama Kenya ama Tanzania. Bi. Spika wa Muda, ningependa kutoa himizo kwa sisi viongozi ambao tuna nafasi za uongozi na tuko katika siasa ya kwamba tunapopata fursa kama hizi; na sisi wakati mwingi huwaita viongozi wa serikalini, mawaziri ama makatibu wa kudumu, hapa lakini hatujawai kuwa na mawazo ya kuwasukuma kuwauliza, “Je, ninyi mmefikisha wapi mazungumzo haya ya kuangalia kwamba katika miaka mingine 20 inayokuja, Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki iwe kitu kimoja?” Twakumbuka kwamba kule zamani kabla sijazaliwa, pengine viongozi wengine walio hapa walikuwa wamezaliwa wakati huo, mimi husikia tu kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjika kwa sababu Wakenya walifanya vile, Watanzania walifanya vile na Waganda walikuwa na haya. Mimi nina imani kwamba tukifuata mwelekezo ambao sisi tulipewa na Rais Suluhu Hassan, tutaweza kuungana tena na wakati huo biashara zetu ambazo mingi ziko hapa Kenya na kule Tanzania zitaweza kuwa na nguvu zaidi kuliko inavyopatikana hivi sasa. Bi. Spika wa Muda, yangu nikumalizia na kusema tafadhalini, sisi kama viongozi tukishapewa fursa kama hii na kuelezwa mawazo mazuri kama yale, tujihimize na tuangalie ni vipi tunaweza tukatekeleza yale mapendekezo aliyotupa kwa upande wetu. Yeye alisema ninyi kama Wakenya lindeni upande wenu. Mimi ninawahikikishia nikiwa Rais wa Tanzania kwamba moja ya agenda zile nitahakikisha nimestawisha na kunawiri chini ya uongozi wangu ni Jumuiya hii ya Afrika Mashariki. Natumai katika wiki ambazo zinakuja, Rais wa Jamhuri ya Kenya atakuja kutupa hotuba ambayo anatupa kila mwaka. Moja ya mambo ambayo lazima wale ambao wanaandika hotuba yake watuletee katika Bunge hili kwa sababu najua wanafuatilia mazungumzo haya ni vipi na mikakati ipi ambayo Rais wetu, Rais Uhuru Kenyatta, ametia katika mipango yake kuhakikisha kwamba kuna uwiano mzuri kati ya jamii hizi ambazo zinaishi na nchi hizi ili sisi wote tuweze kustawi na tuwe na Jumuiya njema. Bi. Spika wa Muda, nashukuru. Namkaribisha tena aje kwa sababu wakati alikuja kulikuwa na furaha sana nchini. Mgeni huyo azidi kuja ili sisi tupone. Asante, Bi. Spika wa Muda."
}