GET /api/v0.1/hansard/entries/1073034/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073034,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073034/?format=api",
    "text_counter": 208,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Sikuwa nimepanga kuzungumza kwa Lugha ya Kiswahili lakini kama Sen. Cheruiyot anaweza kuzungumza Kiswahili, hakuna yule ambaye hawezi. Bi. Spika wa Muda, wajua katika taifa letu tuko na wale ambao ni Nilotes, Bantus na Cushites. Wale ambao wametoka katika ukoo wa Nilotes wakizungumza Kiswahili kwao ni changamoto kubwa sana. Haswa, wakijaribu wanaweza kujikwaa au kuteguka. Ni ngumu sana hasa kwa wale wametoka Nyanza. Lakini hata sisi wengine tukijaribu wengine wetu tumezaliwa Nairobi na Kiswahili chetu ni kile cha mtaa. Nakumbuka Rais Suluhu akisema ana enjoy akisikia tukizungumza Kiswahili chetu. Ningeomba Sen. Madzayo, Seneta wa Kilifi na wale walio na uzoefu wasitukosoe sana kwa sababu watafanya tufe moyo na tusiwe tunajaribu kuzungumza kwa Kiswahili. Bi. Spika wa Muda, pia mimi nitajaribu kuchangia Hoja hii ambapo tunatoa shukrani ya Seneti kwa Rais wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan kwa hotuba ambayo alitoa katika Bunge letu kwa Kikao cha pamoja wa Bunge la Kitaifa na Seneti ambayo tulihudhuria sote au baadhi yetu. Rais Samia Suluhu alitamatisha hotuba yake kwa kutupa baraka kubwa kwa kusema hudumu undugu wa Wakenya na Watanzania. Alisema wadumu viongozi, Mungu aibariki Jamhuri ya Kenya na Mungu aibariki Jamhuri wa Muungano wa Tanzania. Bi. Spika wa Muda, nilifurahi sana kukutana na Rais wa Tanzania alipokuja kwa sababu nilikuwa miongoni wa wale viongozi ambao walimpokea kama Seneta wa Nairobi. Kabla ya kutoa Hotuba yake, tulipata muda kidogo wa kuzungumza naye. Rais Suluhu alinishangaza sana kwa sababu alikuwa na utulivu sana. Sio kawaida ya Rais. Alikuwa anataka kujua mambo mengi. Aliuliza kuhusu jinsi Maseneta huchaguliwa. Nakumbuka alishangaa sana alipoelezwa mimi ni Seneta wa Nairobi. Aliniuliza iwapo nilichaguliwa Nairobi nzima. Alishangazwa na umri wangu. Lakini nilimweleza kwamba tulikuwa tunafuatilia uongozi wake. Baadaye, Sen. Madzayo alikuwa na sisi. Tulimweleza kwamba tumekuwa tukiwasiliana na viongozi wengine katika Jamhuri ya Tanzania na kuwa sisi ni marafiki. Kwa mzaha, tulimwambia kwamba hatutaki arudi Tanzania ila abakie Kenya kwa sababu tulikuwa na furaha sana kumwona. Bi. Spika wa Muda, Rais Samia Suluhu aligusia mambo muhimu sana. Kwa vipengele ambavyo alizingatia, jambo muhimu alilogusia ni kwamba, nchi yoyote"
}