GET /api/v0.1/hansard/entries/1073036/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1073036,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1073036/?format=api",
    "text_counter": 210,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Sakaja",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13131,
        "legal_name": "Johnson Arthur Sakaja",
        "slug": "johnson-arthur-sakaja"
    },
    "content": "ulimwenguni inaweza kubadilishwa kwa muda mchache sana kwa sababu ya kiongozi mmoja. Bi. Spika wa Muda, Rais Samia Suluhu hajakuwa Rais kwa muda mrefu. Hapo awali kulikuwa na fikra ambazo hazifai kati ya nchi zetu, lakini kwa muda mfupi sana, taswira au mandhari ya kisiasia na uhusiano wetu umebadilika. Amerudisha matumaini kwamba, Kenya na Tanzania ni nchi zinazoweza kuangaliana kama ndugu. Tuna mengi ambayo tunakubaliana nayo kuliko yale ambayo hatukubaliani nayo. Bi. Spika wa Muda, alinikumbusha kuhusu Waziri Mkuu wa Singapore, Lee Kwan Yew, ambaye alibadili nchi ya Singapore. Jirani wao wa Malaysia walikuwa wamekataa kuungana nao. Alisema kwamba hakuna shaka wataweza kustawi kama nchi. Alibadilisha nchi yake. Rais wa Rwanda ameweza kuinua nchi yake ya Rwanda baada ya vita au uhusama. Ni nchi ambayo watu wengi wanatamani au ni mfano ambao unaweza kufuatwa na nchi zingine. Nilifurahi na nilipata matumaini kwamba uongozi--- Mwandishi John Maxwel alisema kuwa kila kitu huanza na kukamilika na uongozi. Uongozi ndio unabadilisha maisha ya watu na nchi. Nampongeza sana. Nilifurahi nikimwangalia Rais Suluhu kwa sababu mtoto wangu wa kike anaweza kuwa na matumaini ya kuwa Rais siku moja. Sisi kama taifa tumekuwa tunasema kina mama lazima wapate nafasi ya uongozi. Rais Suluhu ni mfano mzuri sana. Uongozi bora unaweza kutoka kwa mwamamme au mwanamke. Tunamtakia kila la heri Rais wa Tanzania kwa kazi kubwa ambayo anayo. Mojawapo ya sheria arobaini na nane za uongozi au 48 laws of power, inasema usijivishe viatu vya kiongozi mkubwa. Yeye amefuata kiongozi ambaye alikuwa kiongozi imara na shupavu, Dr. John Pombe Magufuli. Nina uhakika na amani kwamba Rais Samia Suluhu anaweza, anatosha na ataendelea kuongoza Taifa la Jamhuri ya Tanzania. Bi. Spika wa Muda, ni jambo la busara ambalo sisi kama Wakenya tunafaa kufurahia. Hii ni kwa sababu Rais Suluhu alisema kwamba ilikuwa ni ziara yake ya kwanza rasmi kama Rais, kuja Kenya. Yeye ndio Rais wa tatu tangu Bunge la kwanza la Kenya kuja kutoa Hotuba Rasmi katika Bunge la Kenya. Wa kwanza alikuwa Rais wa Nigeria Jonathan Goodluck. Wa pili alikuwa ni Rais Kikwete. Alitoa Hotuba Rasmi katika kikao cha pamoja cha Bunge la Kenya. Wa tatu ni Rais Samia Suluhu.Tunamshukuru sana. Kenya inaheshimika sana. Alikiri kwamba alipata mapokezi mazuri na alifurahia kuwa Kenya. Hii ni kwa sababu kadhaa alizotaja. Ya kwanza ni undugu wa damu ambao upo kati ya Wakenya na watanzania. Mipaka yetu ni bandia. Ni mipaka ambayo haikuwa. Aliorodhesha majina kama Otieno, Oboke, Namelock ambayo yako Kenya na Tanzania. Pia, alitaja ndugu yetu Seneta wa Mombasa. Alisema jina Faki Mohamed Mwinyihaji ni jina la Kizanzibari. Mhe. Faki alifurahi sana kuwa Rais wa Tanzania anamjua.Tuko na umoja wa ukoo au undugu wa damu. La pili, ni historia kati ya Kenya na Tanzania tangu kuzinduliwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka wa 1967. Nakumbuka Spika wetu alipata shida kidogo kutamka tarehe kwa Kiswahili. Nchi zetu zimekuwa na uhusiano katika East Africa CommonServices organization, zikiwemo nchi za utawala na ukoloni wa Waingereza. Kenya na Tanzania inahitajiana."
}